Wakaazi wa jimbo la Somaliland wapiga kura kumchagua rais na wabunge
Manage episode 449974716 series 1091037
Wakaazi wa jimbo la Somaliland, mojawapo wa êneo lililojitenga na Somalia zaidi ya miaka 30 iliyopita, tangu mwaka 2003 wamekuwa wakishiriki kwenye uchaguzi wa kumchagua rais na wabunge wao.
Fursa hiyo pia imekuja Novemba tarehe 13 mwaka 2024 ambapo wapiga kura Milioni 1 waliondikishwa na Tume ya Uchaguzi ya Somaliland wanamchagua rais atakayewatumikia kwa miaka metano.
Wagombea watatu wanatafuta urais wa jimbo hilo, akiwemo kiongozi wa sasa Muse Bihi Abdi, anayetaka muhula wa pili, lakini mpinzani wake mkuu ni Abdirahman Mohamed Abdullahi, maarufu kwa jina la "Irro,”.
Kwenye Makala ya Wimbi la Siasa, tunajadili umuhimu wa uchaguzi wa jimbo la Somaliland na umuhimu wake, kwenye Jumuiya ya Kimataifa, wakati huu, êneo hilo linapotaka kujitawala.
24 פרקים